Je, utambulisho wa mtoa taarifa utalindwa/utahifadhiwa?
Fomu ya kutolea taarifa ni ya siri na haina utambulisho wo wote. Ili kuzuia kutambuliwa kwa mtoa taarifa hatuhitaji maelezo yanayoweza kumtambulisha.Tunapenda kukutahadharisha kwamba utakapomaliza kujaza fomu usiweke taarifa zo zote zinazoweza kukutambulisha.
Je, kuna ye yote, ikiwa ni pamoja na GHI watakaojua kuwa nimetembelea ukurasa wa watoa taarifa na kujaza fomu?
Seva ya GHI inakusanya anuani za IP kwa wanaotembelea tovuti yao. Anuani ya IP ni anuani ya kipekee inayoweza kutambua kifaa kilichotumika kwenye mtandao na mahali kilipotumika (mji, nchi). Pia inatambua nani analipia gharama za mtandao kwa kifaa husika. Hivyo, kama unatumia kompyuta yako binafsi, hizi taarifa zitaonyesha kwamba kumputa yako imetumika, japokuwa haitaonyesha ni nani alitumia. Kwa sababu hiyo ni vema kutumia kompyuta zilizotengwa kwa matumizi ya umma kama intaneti Kefu ama kuipata fomu kwa kutumia mfumo binafsi wa intaneni usiyo bayana -virtual private network ama VPN. VPN imewekwa kama programu ya kompyuta kwenye kifaa chako. Utakapo ipata fomu kwa njia ya VPN, inaelekeza muunganisho wa intaneti yako kama vile haupiti katika kompyuta yako na hivyo kuufanya salama na kukuwezesha kuutumia bila kutambulika.
Je, mwajiri wangu atajua kwamba nimetembelea ukurasa wa watoa taarifa na nimejaza fomu?
Baadhi ya makampuni yanaweza kutambua ni komputa zipi zimetumika kutembelea tovuti ya mtoa taarifa, zikiwa bado zimeunganishwa kwenye mtandao. Kwa jinsi hiyo, unaweza kutambuliwa na makampuni hayo. Hivyo, kuna baadhi ya vifaa kinga/njia salama tunashauri uzifuate:
- Usitumie simu au kompyuta ya kampuni
- Usitumie mtandao wa kampuni
- Fungua tovuti kwenye kichupo cha faragha ama ukurasa (window) usiotambulika na hii itazuia tovuti uliyotembelea kutoonekana kwenye historia ya kivinjari
- Chrome:Windows, Linux, au Chrome OS: Bonyeza Ctrl +Shift + n, Mac: Bonyeza ⌘ + Shift + n
- Firefox: Windows, Linux: Bonyeza Ctrl +Shift + p, Mac: Bonyeza ⌘ + Shift + p
- Safari: Mac: Bonyeza ⌘ + Shift + n
- Edge: Windows, Linux: Bonyeza Ctrl + Shift + p , Mac: Bonyeza ⌘ + Shift + n
Kama utachukua tahadhari hizi, sio rahisi kujua kwamba ulishawahi kutuma fomu.
Je, fomu ya mtoa taarifa inatumia vidakuzi na je, watanitambua?
Tovuti hii na fomu ya mtoa taarifa hazitumii vidakuzi.
Je, kuna uwezekano mtu mwingine kudaka/kuingilia taarifa ninazoingiza kwenye fomu?
Taarifa zinaweza kuingiliwa kwa muda mchache wakati ukituma fomu na maudhui kuhamishiwa kwenye seva yetu. Hata hivyo maudhui ya fomu yamesimbwa kwa njia fiche (kwa kutumia HTTPS) na hivyo, endapo mtu ataingilia mkondo wa data, hataweza kutambua ama kufafanua maudhui yaliyomo.
Pindi fomu ya data inapotumwa GHI, inawekwa sehemu tofauti na taarifa za anuani ya IP, kifaa na mtandao uliotumika. Inahifadhiwa kwenye seva salama, na inayotumika kwa kazi hiyo tu. Seva hii ipo, chini ya mamlaka na uangalizi wa Umoja wa Ulaya na kwa kuzingatia sheria za Umoja wa Ulaya. Kwa hali hii, itakuwa vigumu kuhusisha fomu na chombo ama mtandao ulitomika.
Je, taarifa nitakazotoa, zitatumikaje?
Taarifa zisizokuwa na utambulisho wa mtoa taarifa hupelekwa kwa wataalamu walioteuliwa na GHI kwa uchambuzi. Kama wataalamu hao watabaini kwamba ripoti iliyopokelewa inahitajika kufanyiwa kazi kwa sababu za usalama wa chakula, tahadhari itapelekwa kwenye mamlaka za usalama wa chakula, kwenye nchi husika pamoja na ushauri wa kuchunguza tukio lililoripotiwa.